BONDIA ALBERT MENSAH KUWA NA WAKATI MGUMI ULINGONI TAREHE 30, MACHI
Albert Mensah (kulia) akifanya
anachokipenda sana “Kuwaadhibu wapinzani
wake”
FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 1st, 2013
-Dar-Es-Salaam, TANZANIA-
Bondia wa IBF aliye na kiwango cha namba 11 duniani katika uzito Jr. Welter, Albert Mensah wa Ghana atakuwa kwenye wakati mgumu atakapombana na bondia mkongwe ulingoni na asiye na huruma na ngumi zake Mghana Ben Odamettey katika mpambano wao wa kugombea mkanda wa “IBF Africa uzito wa jr. Welter”.
Bondia wa IBF aliye na kiwango cha namba 11 duniani katika uzito Jr. Welter, Albert Mensah wa Ghana atakuwa kwenye wakati mgumu atakapombana na bondia mkongwe ulingoni na asiye na huruma na ngumi zake Mghana Ben Odamettey katika mpambano wao wa kugombea mkanda wa “IBF Africa uzito wa jr. Welter”.
Pambano hili linalowafanya Waghana wengi kuwa na roho juu juu
kuhusu ni nani haswa mbabe kati ya wawili hao litafanyika jijini Accra, Ghana
tarehe 30 Machi 2013 na linaandaliwa na kampuni kubwa ya kupromoti ngumi ya “GoldenMike
Boxing Promotions Syndicate” inayomilikiwa na bwana Michael Tetteh and Henry
Many-Spain.
Huu ni wakati ambao Waghana wengi kutoka kila kona ya nchi
waliokuwa wanaungojea na wawili hao hawajaacha kugeuza hata jiwe moja kwa namna
wanavyojifua kwa mazoezi yao ya mpambano huu!
Albert Mensah, ni bondia mtulivu na anayetumia akili nyingi
ulingoni ambaye mabondia wengi waliokutana naye wanakiri kuwa huwezi kujua
anachokifikiri ukingoni na hata ni ngumi gani atairusha kwako na wakati gani. Ni
bondia aliyepewa nafasi kubwa sana ya kuchukua umaarufu wa bondia bingwa wa
zamani wa dunia wa Ghana Profesa Azumah Nelson.
Naye bondia mwenye madaha na majivuno mengi Ben Odamettey, huu
ni wakati wa ukweli umewadia kwani atatakiwa kuwahakikishia wapenzi wake kuwa
hana wasiwasi na mpambano huu na kwamba yuko tayari kukumbana na adui wake
mkubwa ambaye ni “Hasira”
Wakati ambao Waghana wa kila umri na rika zote waliokuwa wanaungojea
na hawatangoja zaidi ya tarehe 30 Machi, 2013.
Usitike kweney ukurasa huu kwa habari zaidi…..!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION
AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment