March 25, 2013

KAJALA IS NOW FREE
 
STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja leo ameokolewa na Wema Sepetu kwenda jela miaka mitano baada ya Wema kulipa faini ya milioni 13 aliyotakiwa kulipa Kajala,hukumu iliyotolewa leo jijini Dar Es Salaam na Hakimu Mkazi Mahakama ya Kisutu .Aidha Mume wa Kajala Faraji Agustino alitakiwa kulipa faini ya Milioni 200 au kwenda jela miaka 7.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.

Awali mwaka jana Mwezi Machi,inadaiwa kuwa familia ya Kajala ilikataa Wema kutoa fedha kwa ajili ya kumdhamini asiende jela lwa madai kuwa walikuwa hawahitaji msaada kutoka kwa msanii mwenzake huyo.

No comments: