CORD wadai mizengwe kwenye uchaguzi Kenya
MUUNGANO wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua za kuchukua kufuatia madai ya hujuma katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu.
Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza
kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais
kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa
Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema
kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais
kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa
makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Musyoka vile vile amesema kuwa muungano huo una tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo wakisema sio ya kweli.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana
na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na pia kuanza upya kwa shughuli ya
kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani.
Musyoka alisema kuwa tume ya uchaguzi inastahili
kutumia mitambo ya elektroniki kuhesabu kura kama inavyoagiza katiba ya
nnchi, huku akiongeza kuwa muungano huo ungali unatafakari hatua za
kuchukua ingawa kwa kufuata sheria.
Moja ya hatua inazotafakari kuchukua ni kwenda mahakamani kuitaka mahakama kusimamisha shughuli ya kuhesabu kura na kuanza tena.
No comments:
Post a Comment