JK- Tunajua biashara ya dini inalipa, lakini msiivuruge Tanzania
RAIS
Jakaya Kikwete amesema kuwa mtindo wa kufanya fujo na kusababisha
uvunjifu wa amani kwa visingizio vya dini nchini ni biashara inayolipa
na ndiyo maana wakereketwa wa kufanya hivyo hawaishi.
Hata hivyo, akaonya kwamba Serikali katu haitawavumilia wanaotaka kuwavuruga Watanzania kwa kutumia dini zao.
Kikwete
aliyasema hayo wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mchakato wa Nchi za
Afrika Kujitathmini zenyewe katika nyanja za Demokrasia, Utawala Bora na
Uchumi (APRM) nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema
ni jambo la kushangaza kuona kuwa wadau wanatumia dini kuiyumbisha nchi
kwa vigezo kuwa ni miongoni mwa nchi zilizodumisha amani kwa muda
mrefu.
Alisema
kutokana na hali hiyo, Serikali yake haitayumba wala kusita kupambana
ipasavyo na wafanya fujo hao ikiwa ni pamoja na kutumia njia za busara
wakati wa kutoa uamuzi na hatua za kisheria.
“Kuna
baadhi ya watu wanatumia vigezo vya kidini kwa ajili ya kufanya vurugu
za kuhatarisha amani, Serikali haitaweza kuwavumilia, badala yake
tutatumia njia mbalimbali ili kushughulikia matatizo hayo ikiwa ni
pamoja na kutumia busara na hatua za kisheria,” alisema Kikwete.
Alisema mapendekezo yaliyotolewa na APRM ya kusimamia kwa uangalifu tofauti za kidini nchini ameyachukua kwa mikono miwili.
Alisema
kitendo cha Tanzania kuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ni bahati
iliyotokana na kutokuwapo kwa ugomvi wa kikabila, kidini ama yale ya
kutokana na rangi za watu. Alisema hali hii inatokana na ukweli kuwa
sera iliyopo haina ubaguzi kwa wananchi kwa misingi ya kabila, dini,
rangi ama sehemu anakotoka Mtanzania, ni sera nzuri na wanaidumisha.
Kwa
mujibu wa Kikwete, uzuri kuhusu dini katika Tanzania ni kwamba kila
mmoja ana uhuru wa kuabudu na kwamba Serikali haina dini.
“Tunajua
fika kuhusu hatari zinazoweza kusababishwa na baadhi ya wanasiasa na
viongozi wa dini wenye malengo ya kuchochea fujo za kidini, hatuwezi
kuyumba wala kusita kupambana ipasavyo na watu wa namna hiyo,”
alibainisha.
Alisema
ikiwa wataona uchochezi wa kidini unafikia kiwango cha kuhatarisha
amani ya nchi ama uvunjifu wa amani na sheria na dola itachukua mkondo
wake ili haki iweze kutendeka.
Mwananchi
.jpg)

No comments:
Post a Comment