WANANCHI wa kijiji cha Itununu kata ya Nyamoko wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara wamemuua mkazi wa kijiji hicho kwa kipigo kisha kumchoma mto mwili wake baada ya kukamatwa kwa tuhuma za wizi wa kutumia
funguo.
Tukio hilo limethibitishwa na uongozi wa kijiji ,kata na polisi wilayani linadaiwa kutokea januari 26,majira ya usiku katika kitongoji cha Manyata mwaka huu.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Jakobo Mbota alimtaja aliyeuawa kuwa ni Nchore Nyakiha(35)mkazi wa kijijini hapo aliyekufa kutokana na kipigo kikali kutoka kwa wakazi hao baada ya kubainika kuiba kwa kutumia
funguo.
“Januari 25 majira ya saa 1:00 asubuhi Marwa Waisare mwenye duka lililoibiwa alifungua duka na kukuta vitu vimeibiwa na kupiga yowe na wananchi wakajitokeza huku wakiwa na silaha za jadi”alisema.
Baada ya kupata maelezo walianza kufuatilia nyayo hadi nyumbani kwa huyo marehemu na kumweleza jinsi wanavyomtuhumu ,hata hivyo alikataa wakaanza kubishana kwa muda wa zaidi ya masaa mawili ,hatimaye akakiri
kuhusika.
“Aliruhusu upekuzi wakapata vitambaa vya aina mbalimbali ndani ya mfuko ameweka juu ya dari …hapo hapo wakajichukulia sheria mkononi na kuanza kumpiga kisha wakambebesha mfuko kuelekea ofisi ya serikali ya kijiji”alisema Mbota.
Hata hivyo hawakufika ofisini na kuanza kumshambuliwa kwa kipigo walipoona amezidiwa wakamchoma moto kisha wakatelekeza mwili wake
njiani.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Samweli Ryoba alipoulizwa kwa njia ya simu alisema wakati wanatekeleza mauaji hayo hapakuwa na kiongozi wa serikali ya kijiji hicho.
“Nyuma ya uamzi wa wananchi kuna mambo ambayo yalikuwa yakimzunguka marehemu huyo…maana alikuwa natuhuma za wizi wa ng’ombe,kutumia funguo bandia na kuvunja maduka ya watu…taarifa ambazo hata ofisi yake inazo na hivi karibuni alikamatwa kwa wizi wa ng’ombe 6 kutoka kijiji cha Kenyana”alisema.
Na kuwa amewahi kufukuzwa kijijini hapo akiwa na wenzake wananchi waliwachomea nyumba zaidi ya 60 kutokana na kaya nane na kulazimika kuhama kijijini hapo na hali ikatulia.
Hata hivyo watu waliofukuzwa kwa tukio hilo waliomba msamaha kupitia ritongo na kuahidi kutojihusisha na wizi tena ,jambo la kushangaza umezuka tena wa kutumia funguo za bandia na kuwa sasa wanategemea kufanya mkutano wa ritongo ili kukomesha vitendo hivyo.
Kuhusu thamani ya vitu vilivyoibiwa alidai vina kisiwa kufikia zaidi
ya shilingi milioni 2,ikiwemo nguo za kiume ,watoto na wanawake.
Baadhi ya wananchi walisema kuwa uamzi huo unatokana na watuhumiwa wa wizi kuwa na mitandao hadi kwenye vyombo vya dola ambapo huachiwa kila wakikamatwa na kuwa njia pekee ni kuwaua.
Hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo.

No comments:
Post a Comment